IQNA

Ayatullah Bahjat, nembo ya elimu, takwa na uchaji-Mungu

15:50 - May 20, 2009
Habari ID: 1781006
Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu nchini Iraq limetoa taarifa ya rambirambi na kuelezea masikitiko yake makubwa kutokana na kifo cha Ayatullah Muhammad Taqi Bahjat.
Limesema katika taarifa hiyo kwamba, Alim huyo alikuwa nembo ya irfan, takwa na uchaji Mungu katika ulimwengu wa Kiislamu. Huku likitoa mkono wa rambirambi na pole kwa Imam wa Zama (af), maraji' watukufu, vyuo vya kidini na umma wa Kiislamu, baraza hilo la Iraq limeendelea kusema kuwa, mwanazuoni huyo mashuhuri alitumia umri wake wote katika kutetea neno la haki, kueneza elimu ya Kiislamu na kuhudumia madhehebu ya utukufu na uongozi wa Watu wa Nyumba ya Mtume (saw). Limesema vyuo vya kidini vimefaidika mno na elimu na vitabu vyenye thamani kubwa vya mwanazuoni huyo. Mwishoni limewatakia rehema ya Mwenyezi Mungu, utulivu na subira jamaa na familia ya mwanazuoni huyo. 407588
captcha