IQNA

Bustani ya Qur'ani Tukufu kutengenezwa mjini Dubai

15:52 - May 20, 2009
Habari ID: 1781007
Meya wa mji wa Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu ametangaza habari ya kutengenezwa bustani ya Qur'ani Tukufu katika eneo la al-Khawanij katika mji wa Dubai.
Amesema utengenezaji wa bustani hiyo ni moja ya miradi muhimu ya Dubai na kwamba katika bustani hiyo mimea mbalimbali ya dawa, matunda na ile iliyotajwa kwenye kitabu kitakatifu cha Qur'ani itapandwa na kukuzwa.
Mbali na mimea hiyo iliyotajwa kwenye Qur'ani, idara ya meya wa mji huo pia ina nia ya kutekeleza katika bustani hiyo baadhi ya miradi ya masomo ya kimaanawi na visa mbalimbali ambavyo vimetajwa katika Qur'ani Tukufu. Lengo la kutengenezwa bustani hiyo ni kuwafahamisha zaidi watalii na wanaotembelea bustani hiyo mafundisho na madhumuni ya Qur'ani Tukufu. Bustani nyingine kama hiyo ilianzishwa huko mjino Doha Qatar kwa ushirikiano wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO. 407614
captcha