IQNA

Mapambano ya Ummah wa Kiislamu yamemlazimu Obama kubadili sera

8:17 - June 09, 2009
Habari ID: 1788899
Hotuba ya Rais Barack Obama wa Marekani huko Cairo Misri ambapo alisema atabadilishia sera za nchi yake kuhusu Waislamu na Ulimwengu wa Kiislamu inatokana na mapambano endelevu ya Umma wa Kiislamu.
Kwa mujibu wa Tovuti ya saffar.org, Sheikh Hassan al Saffar, msomi wa Kishia nchini Saudi Arabia amedokeza hayo na kuongeza kuwa: "Mwamko wa Ummah wa Kiislamu umefika kiwango cha juu na hivyo kuzima njama za maadui". Mwanachuoni huyo amesema Obama ametoa matamshi ya kubadili sera za Marekani lakini hana uwezo wa kutekeleza kivitendo ahadi zake. Sheikh Saffar ameshangaa kuona baadhi ya wahubiri wa Kisalafi katika ulimwengu wa Kiislamu wakikaribisha hotuba iliyojaa hadaa ya Obama katika Chuo Kikuu cha Cairo.
Sheikh Saffar amesema ingawa hotuba ya Obama nchini Misri ilikuwa na nukta chanya, lakini Marekani inapaswa kubadilisha sera zake zisizofaa kuhusiana na mapambano dhidi ya ugaidi. Mwanazuoni huyo wa Saudi Arabia amesema Waislamu wanaochukizwa na hatua ya Marekani ya kuendelea kuunga mkono jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina.
Itakumbukwa kuwa tarehe 4 Juni rais Obama alitoa hotuba katika Chuo Kikuu cha Cairo na kusema Marekani inataka kufungua ukurasa mpya na ulimwengu wa Kiislamu. Weledi wa mambo wanasema hotuba hiyo ilikuwa ni mkakati wa kusafisa sura iliyochafuka ya Marekani na kwamba Obama hana uwezo wa kutosha kutekeleza kivitendo aliyoyasema. 417826

captcha