Jumuiya hiyo inadai kuwa sababu ya kupinga ujenzi huo ni uhusiano ulipo baina ya Baraza la Waislamu la Poland linalosimamia ujenzi huo na harakati ya Ikhwanul Muslimin inayutuhumiwa kwamba ina misimamo mikali.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Taasisi ya Ibn Khaldoun ya Poland Boguslav Zadorsk amekanusha madai hayo akisema kuwa Baraza la Waislamu la nchi hiyo ni taasisi iliyoundwa na Wapolandi wenyewe na kwamba hadi sasa hakuna chombo chochote kilichowahi kulituhumu baraza hilo kuwa limekiuka sheria za nchi. Boguslav Zadorsk ameongeza kuwa tuhuma za kuwa na uhusiano na harakati ya Ikhwanul Muslimin hazina msingi wowote.
Mwanachama wa Halmashari ya Jiji la Warsaw Tomasz Andryszczyk amesema ujenzi wa msikiti huo unafanyika kwa njia za kisheria na kwa mujibu wa ruhusa ya Halmashari ya Jiji na kwamba makubaliano ya ujenzi wake yalipitishwa kitambo.
Idadi ya Waislamu nchini Poland inakadiriwa kuwa ni zaidi ya elfu 40, elfu 13 miongoni mwao wanashi mjin Warsaw. Kuna misikiti mitatu tu nchini humo. 555115