IQNA

Oman kuandaa kikao cha Kimataifa cha Fiqhi

11:03 - April 04, 2010
Habari ID: 1902075
Kongamano la Kimataifa cha "Fiqhi ya Ustaarabu na Maendeleo" litafanyika hivi karibuni nchini Oman.
Wasomi na wanazuoni 44 kutoka nchi mbali mbalu duniani watashiriki katika kongamano hilo litakalofanyika Muscat, mji mkuu wa Oman.
Kati ya wanaotazamiwa kushiriki ni Mkuu wa Taasisi ya Utamaduni na Sayansi za Kiislamu ya Iran Hujjatul Islam Ahmad Mobaleghi, Mufti wa Oman na Katibu Mkuu wa Jopo la Masomi ya Kiilamu ya Chuo Kikuu cha Al Azhar cha Misri.
Mada muhimu zitakazojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na "Fiqhi ya Mazingira", "Fiqhi ya Kazi na Masoko", "Fiqhi ya Maumbile", "Fiqhi ya Ubinaadamu" na "Fiqhi ya Maendeleo".
556614
captcha