Mashindano ya Quran Tukufu kote duniani yanapaswa kuwa na nafasi muhimu katika kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu, amesema Mfalme wa Malaysia, Mizan Zainul Abidin.
Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Quran IQNA, Mfalme huyo ameyasema hayo alipohutubia kikao cha ufunguzi wa Mashindano ya 52 ya Kimataifa ya Quran Tukufu mjini Kuala Lumpur.
Ameongeza kuwa mashindano hayo yamefanyika kwa lengo la kuimarisha mshikamano wa Kiislamu na kuhuisha Sunnah ya Mtume Muhammad SAW.
'Katika ulimwengu wa leo, ni jambo la kusikitisha kuwa kuna dhana potofu kuhusu Uislamu. Ni wajibu wa nchi za Kiislamu kuungana na kujitahidi kuimarisha roho halisi ya Uislamu na kuwasilisha taswira sahihi ya dini hii tukufu ulimwenguni', amesema Mfalme wa Malaysia, Mizan Zainul Abidin.
Mfalme huyo amemaliza hotuba yake kwa kusistiza kuhusu udharura wa kuimarisha Umoja wa Kiislamu.
622250