IQNA

Usanifu majengo wa misikiti ya Syria kuchunguzwa

12:23 - August 04, 2010
Habari ID: 1966746
Kongamano la usanifu majengo wa misikiti ya Syria iliyojengwa wakati wa utawala wa Othmaniya limefanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Damascus.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo limefanyika chini ya anwani ya “Waarabu na Waturuki, Mkondo wa Historia na Utamaduni.
Muhamad Zeinul Abidin mmoja kati ya wahandisi wasanifu majengo nchini Syria alitoa hotuba kwewnye kongamano hilo akiwafafanulia washiriki kuhusu mbinu ya usanifu majengo wa Syria katika zama za utawala wa Othmaniya.
Amesema sifa muhimu zaidi za misikiti katika zama za Othmaniya nchini Syria zilihusu namna ya matumizi ya vifaa vilivyostawi katika ujenzi wa misikiti.
Kongamano hili limefanyika kwa hisani ya Kituo cha Utafiti wa Utamaduni, Sanaa na Historia cha Syria kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC. Mkutano huo wa siku mbili uliomalizika tarehe mbili Agosti umehudhuriwa na wataalamu wa Syria na Uturuki.
625908
captcha