Kwa mujibu wa ripota wa IQNA, mashindano hayo ya kuhifadhi na kuisoma Qur'ani Tukufu yatafanyika katika makundi sita tafauti. Kutakiwa na kitengo cha kuhifadhi suratul Kafirun maalumu kwa watoto wenye umri miaka 3-4, kuhifadhi Ayatul Kursi kwa ajili ya watoto wenye umri wa miaka 5-6, kuhifadhi sura Dhuhaa kwa ajili ya watoto wenye umri wa miaka 8-7 , kuhifadhi suratul Fajr kwa ajili ya watoto wa miaka 9-10 na kusoma Qur'ani Tukufu maalumu kwa vijana walio na umri wa miaka 11-15 na vile vile kwa ajili ya walio na umri wa juu ya miaka 16.
Katika kitengo cha kuhifadhi dua, mashindano hayo yatawashirkisha vijana walio na umri wa miaka 10-14. Washindi watatunukiwa zawadi katika sikukuu ya Idul Fitr.
625924