IQNA

Redio ya kwanza ya Qur'ani kuzinduliwa nchini Mauritania

19:34 - August 05, 2010
Habari ID: 1967691
Redio ya kwanza ya Qur'ani Tukufu itafunguliwa hivi karibuni nchini Mauritania kwa shabaha ya kueneza zaidi maarifa ya kitabu hicho kitakatifu cha Mwenyezi Mungu kati ya wananchi wa nchi hiyo.
Mwandishi wa shirika la IQNA ameripoti kuwa Rais Muhammad Ould Abdul Aziz wa Mauritana ametoa amri ya kuanzishwa Redio Qur'ani itakayokuwa na vipindi vya Qur'ani na kutangaza habari zote zinazohusiana na kitbu hicho kitakatifu.
Rais wa Mauritania amesisitiza juu ya umuhimu wa kuwapo chombo cha habari kinachozungumzia masuala ya Qur'ani hususan katika mwezi mtukufu wa Ramadani na akasema kuwa kuna mahafidhi, makari na waaalamu wengi wa masuala ya Qur'ani nchini huo ambao hawajatambulika kutokana na udhaifu wa vyombo vya habari.
Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania iko kaskazini magharbi mwa Afrika na mji mkuu wake ni Nouakchott. Eneo kubwa la ardhi ya nchi hiyo ni jangwa na ina jamii ya karibu watu milioni tatu. 626900


captcha