Mkurugenzi wa taasisi ya uchapishaji ya al Mahdi Ali Madadi ameiambia IQNA kwamba taasisi hiyo imewasilisha tafsiri mbalimbali za Qur'ani, vitabu vinavyohusu taaluma ya kitabu hicho na kadhalika katika maonyesho hayo ya Karbala. Vilevile Ali Madadi amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa zawadi ya nakala elfu mbili za Qur'ani kwa serikali ya Iraq ambazo zitazambazwa katika shule mbalimbali nchini humo.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa maonyesho ya vitabu ya Labbaik yalianza Jumatatu iliyopita. Makumi ya taasisi za uchapishaji kutoka Iran zinashiriki katika maonyesho hayo yatakayoendelea kwa kipindi cha wiki moja. 626968