IQNA

Uturuki kutuma walinganiaji huko Tatarstan katika mwezi wa Ramadhani

12:41 - August 07, 2010
Habari ID: 1968275
Maulama wa Uturuki wanatazamiwa kuelekea katika Jamhuri ya Tatarstan katika Shirikisho la Russia katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa lengo la kutoa miongozi ya kidini.
Kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali ya Tatarstan na Idara ya Masuala ya Kidini ya Uturuki, m aimamu wa swala za jamaa wa misikiti ya Uturuki watatumwa kusalisha katika misikiti ya Tatarstan katika mwezi mkukufu wa Ramadhani.
Aidha maulamaa hao wa Uturuki watakuwa na jukumu la kutoa darsa za Qur'ani na mafunzo mengine ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Jamhuri ya Tatarstan iko katika Shirikisho la Russia lakini ina mamlaka ya kujiendeshea shughuli zake na aghalabu ya wakazi wake ni Waislamu.
627515
captcha