IQNA

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yaanza mjini Tehran

12:48 - August 07, 2010
Habari ID: 1968276
Maonyesho ya 18 ya Kimatiafa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yanafunguliwa rasmi leo Jumamosi katika ukumbi wa sala wa Imam Khomeini.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Qur'ani katika Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu, Hujjatul Islam Hamid Mohammadi, maonyesho hayo yatafunguliwa baada ya sala za Magharibi na Ishaa.
Akizungumza na Shirika la Habari la Qur'ani IQNA, Hujjatul Islam Hamid Mohammadi ameongeza kuwa sherehe za ufunguzi zitahudhuriwa na Ayatullah Mahdavi Kani, Hujjatul Islam Sayyid Ahmad Alamulhuda na Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu Sayyed Muhammad Husseini. Sherehe hizo zitaanza kwa kiraa ya Qur'ani Tukufu itakayosomwa na Saeed Tusi.
Maonyesho ya 18 Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yana washiriki kutoka nchi 25 duniani. Kaulimbiu ya maonyesho ya mwaka huu ni "Qur'ani, Kitabu cha Maisha".
Maonyesho hayo yataendelea hadi tarehe 23 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
627457

captcha