IQNA

Quran Tukufu inazingatiwa katika mipango yote ya serikali ya Iran

9:40 - August 08, 2010
Habari ID: 1968798
Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu Dkt. Sayyed Mohammad Hosseini amesema serikali ya awamu ya 10 ya rais Ahmadinejad inazingatia Quran Tukufu katika mipango yake yote.
Akizungmza Jumamosi usiku katika sherehe za ufunguzi wa Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Quran Tukufu mjini Tehran, Dkt. Hosseini ameongeza kuwa serikali ya awamu ya 10 inazingatia sana masuala ya shughuli za Quran Tukufu nchini. Ameyataja Maonyesho ya Kimataifa ya Quran ya Tehran kuwa tukio lisilo na kifani duniani. Ameelezea matumaini yake kuwa katika siku za usoni maonyesho hayo ya Quran yataenea na kufanyika katika nchi mbali mbali duniani. Itakumbukwa kuwa Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Quran mjini Tehran yana vitengo mbali mbali vinavyohusu Quran Tukufu katika nyanja za Tafsiri ya Quran, elimu, vyuo vya kidini, vitabu, teknolojia, vyombo vya habari vya dijitali, programu za kompyuta, watoto, vijana, familia, mashairi, fasihi, Kaligrafia n.k. Maonyesho hayo ambayo pia yana washiriki kutoka nchi 25 duniani yanafanyika katika ukumbi wa sala wa Imam Khomeini na yataendelea hadi tarehe 23 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
628408


captcha