IQNA

Awamu ya mwisho ya mashindano ya Qur'ani ya wanawake yafanyika Uturuki

16:06 - August 08, 2010
Habari ID: 1969346
Awamu ya mwisho ya mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu makhsusi kwa wanawake imefanyika katika mji wa Bursa nchini Uturuki.
Mashindano hayo ambayo amefanyika chini ya usimamizi wa kitengo cha masuala ya kidini cha Jumiya ya Masuala ya Kiislamu ya Uturuki, yamehudhuriwa na walioshinda katika maeneo nanne ya Uturuki katika Chuo cha Teolojia cha Uludag.
Kila karii katika awamu hii aliulizwa maswali matatu.
Inasemekana kuwa zaidi ya wanawake elfu kumi wa Kiislamu nchini Uturuki wana stashahada za kuhifadhi kitabu kitukufu cha Qur'ani. 627973

captcha