Akizungumza na mwandishi wa IQNA katika ukumbi wa sala wa Imam Khomeini panapofanyika maonyesho hayo, Muhyiddin Abdullah Mohammad amesema: "Mashindano hayo yatafanyika kwa mnasaba wa siku ya kitaifa ya uhuru wa Comoro na yatakuwa katika viwango vya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu".
Amesema mashindano hayo ambayo yatakuwa na vitengo vya wanawake na wanaume awali yatafanyika kieneo na watakaofuzu watashiriki katika mashindano ya kitaifa.
Muhyiddin Abdullah Mohammad amesema mashindano hayo yatafanyika kwa himaya ya Rais Abdullah Sambi wa Visiwa vya Comoro ambaye alisoma katika Chuo Kikuu cha Jamiatul Mustafa (SAW) al Alamiya cha hapa Iran. Ameongeza kuwa washindi wa mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Comoro watashiriki katika mashindano mbalimbali ya kimataifa. 629178