IQNA

Qur'ani ya Dhahabu katika Maonyesho ya Kimataifa ya Kaligrafia ya Russia

15:43 - August 10, 2010
Habari ID: 1970792
Qur'ani ya dhahabu iliyoandikwa kwa mujibu wa nakala ya Othman Twaha itaonyeshwa katika Maonyesho ya Kimataifa ya Kaligrafia yatakayofanyika katika mji wa Velikiy Novgorod nchini Russia kuanzia tarehe 10 hadi 12 mwezi Septemba mwaka huu.
Nakala hiyo ya Qur'ani ya dhahabu yenye thamani kubwa imetayarishwa na taasisi ya Moscow Mint ya ilionyeshwa katika maonyesho ya mwaka jana ya kaligrafia mjini Moscow.
Qur'ani hiyo ya dhahabu imechapishwa kwa mujibu wa nakala ya hati za Othman Twaha inayotambuliwa kuwa ndiyo ya zamani zaidi ya kitabu cha Mwenyezi Mungu. Nakala hiyo ya Othman Twaha inahifadhiwa katika Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Mashariki ya Academia ya Sayansi Russia katika mji wa Saint Petersburg. Nakala hiyo ya Qur'ani yenye uzito wa kilo 14 imetengeneza na kiwanda cha kufua dhahabu cha Moscow kwa kipindi cha miezi 18.
Nakala hiyo ya Qur'ani imekwishaonyeshwa katika nchi za Bahrain, Misri, Libya na maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani ya Tehran. 629475
captcha