IQNA

Saa kubwa zaidi duniani yazinduliwa katika mji wa Makka

13:55 - August 11, 2010
Habari ID: 1971518
Saa kubwa zaidi duniani imezinduliwa leo nchini Saudi Arabia kwa mnasaba wa siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maafisa wa Saudia wanasema saa hii itakuwa inaonyesha saa kwa majira ya Kiislamu yaani Islamic Mean Time (IMT) na kwamba kutoka sasa Waislamu zaidi ya bilioni moja na nusu duniani badala ya kutumia majira ya GMT sasa watakuwa wanatumia IMT.
Saa hiyo yenye sura nne ina mnara wenye urefu wa mita 600 ambao ni wa pili kwa urefu duniani baada ya jengo la Burj Khalifa huko Dubai. Kila upande wa sura ya saa hiyo una maandishi ya “Allahu Akbar” yaliyopambwa kwa maelfu ya taa. Aidha kunaa maandishi ya shahada mbili za "La ilaha ila Allah Mohammad Rasulullah".
Saa hiyo inaweza kuonekana kutoka umbali wa kilomita 25. Wizara ya Waqfu ya Saudia inasema saa hiyo imegharimu dola millioni 800 kujenga.
631156
captcha