IQNA

Qur'ani nzima yaandikwa katika mstari mmoja kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya Tehran

15:47 - August 12, 2010
Habari ID: 1972026
Qur'ani nzima iliyoandikwa kwenye mstari mmoja imeonyeshwa kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya Qur'ani yanayoendelea mjini Tehran.
Qur'ani hiyo ambayo ni ya kwanza ya aina yake ilianza kuandikwa na Muirani Ali Yazdaniyan kwa kutumia kompyuta mwaka mmoja uliopita.
Mwandishi wa mbinu hiyo ya Qur'ani amesema kuwa ameamua kufanya hivyo ili kunufaika na kitabu hicho kitakatifu ambayo ni neema kubwa ya Mwenyezi Mungu kwa mwanadamu na pia kusisitiza juu ya umoja wa umma wa Kiislamu ambayo ni amri muhimu ya Mwenyezi Mungu na mafundisho ya Mtume Wake Mtukufu (SAW).
Maandishi hayo ya Qur'ani yamewavutia watu wengi wanayoyatembelea maonyesho hayo ya Tehran ambayo yamepangwa kuendelea katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. 631642
captcha