Kikao hicho kimeandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Maarifa ya Qur'ani Tukufu cha Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kheri ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Akizungumzia suala hilo, Muhammad Hussein Muslih Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utamaduni na Utafiti wa Qur'ani ya mjini Shiraz amesema wahadhiri mashuhuri watabainisha mitazamo ya Qur'ani kuhusiana na suala muhimu la mazingira kwa kutegemea aya za kitabu hicho kitakatifu.
Mbali na maudhui hiyo, 'nujumu katika Qur'ani' ni maudhui nyingine itakayojadiliwa katika kikao hicho cha kielimu. Amesema washiriki wa kikao hicho watapewa nafasi ya kuulizwa maswali ambayo yatajibiwa na wahadhiri pamoja na wataalamu watakaozungumza katika kikao hicho. Bwana Muslih ameendelea kusema kuwa athari ya Qur'ani kwa washairi wa Iran ni suala jingine litakalojadiliwa katika kikao hicho. 631703