Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini (MA) panapofanyika Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu, tafsiri hizo nadra ni za lugha za Kiurdu, Kiingereza, Kijerumani, Kitaliano, Kibangali, Kikorea, Kifaransa, Kituruki cha Kiazari, Kituruki cha Kiistanbuli, Kirusi, Kiswahili, Kipashtu, Kitamil, Kihindi, Kinorway, Kijerumani na Kikurdi cha Kisurani.
Taasisi ya Kiutamaduni ya Kutarjumu Wahyi ya Iran iliasisiwa mwaka 1995 nchini Iran kwa Ushirikiano wa Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu na Shirika la Wakfu na Masuala ya Kheri.
Lengo la taasisi hiyo ni kuwasilisha tarjumi sahihi na zinazofahamika za Qur'ani Tukufu. Hadi sasa taasisi hiyo imekusanya tarjuma 5300 za watarjumi 1200 wa lugha 112 mbalimbali duniani.
632060