IQNA

Maonyesho ya 'mwaka wa 1400 wa kuteremshwa Qur'ani' kufanyika Uturuki

11:29 - August 14, 2010
Habari ID: 1972701
Maonyesho ya mwaka wa 1400 wa kuteremshwa Qur'ani Tukufu yatafanyika tarehe 5 Septemba mwaka huu katika Jumba la Maonyesho ya Mambo ya Kale ya Sanaa za Kiislamu mjini Istanbul Uturuki.
Gazeti la Zaman la Uturuki ambalo limeandika habari hiyo limesema kwamba zaidi ya nuskha laki mbili na nusu za maandishi ya Qur'ani Tukufu tokea kipindi cha tawala za Waothmania, Wateimuri, Wasafawi, Wailkhani, Banu Abbas na Banu Umayya zitaonyeshwa katika maonyesho hayo.
Vilevile nuskha ya maandishi ijulikanayo kwa jina la Nuskha ya Sham, ambayo imeandikwa kwenye makaratasi yapatayo laki mbili na nusu itaonyeshwa kwa mara ya kwanza katika maonyesho hayo.
Kwa mujibu wa wasimamizi wa jumba lililotajwa la maonyesho ya mambo ya kale, ufunguzi wa maonyesho hayo utahudhuriwa na wahadhiri, wasomi na wataalamu wa mambo ya kale kutoka nchi za Ufaransa, Italia, Ujerumani na Uingerezeza, miongoni mwa wageni wengine. Maonyesho hayo yataonyeshwa kila siku kwa masaa 24 katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. 632141
captcha