IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya wanawake kufanyika Libya

12:41 - August 15, 2010
Habari ID: 1973662
Jumuiya ya Mambo ya Kheri ya ‘Waatasimu’ ya Libya imewaalika wanawake 60 kutoka sehemu mbalimbali duniani kushiriki katika Mashindano ya 6 ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani ya Libya, maalumu kwa wanawake.
Kwa mujibu wa mtandao wa Libya al Youm, Jumuiya ya Mambo ya Kheri ya ‘Waatasimu’ imetangaza kuwa mashindano hayo yatafanyika katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani katika mji mkuu wa Libya Tripoli. Wanawake watakaoshiriki watashindana katika kiwango cha kuihifadhi Qur'ani Tukufu.
Jumuiya hiyo imeongeza kuwa pambizoni mwa mashindano hayo, kutakuwepo programu nyinginezo zitakazowashirikisha wasomi na wanaharakati kutoka ulimwengu wa Kiislamu ambao watatoa hotuba na darsa za kidini katika misikiti ya Libya.
:633556



captcha