IQNA

Muujiza wa kutopotoshwa Qur'ani wathibitishwa tena

15:29 - August 15, 2010
Habari ID: 1973913
Matokeo ya uchunguzi uliofanywa kwa kipindi cha miaka kumi na mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Masala ya Dini ya Uturuki kupitia njia ya kulinganisha nakala ya sasa ya kitabu kitakatifu cha Qur'ani na nakala za kale, yameonesha kwamba hakuna hata herufi moja ya Qur'ani iliyobadilishwa tangu kitabu hicho kiteremshwe hadi hii leo.
Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Masuala ya Dini ya Uturuki Tayyar Altıkulaç amefanya uchunguzi huo wa miaka kumi kwa himaya ya Jumuiya ya Wakfu ya Uturuki na Kituo cha Utafiti, Utamaduni, Sanaa na Historia ya Kiislamu cha Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC).
Amesema kuwa uchunguzi wake ulifanyika kwa kulinganisha herufi kwa herufi na neno kwa neno la nakala ya sasa ya Qur'ani Tukufu na nakala nne asilia zilizoko katika maktaba ya Kituo cha Utafiti, Utamaduni, Sanaa na Historia ya Kiislamu cha Jumuiya ya Nchi za Kiislamu na baada ya utafiti wa miaka kumi imethibitika kuwa kitabu cha Qur'ani hakijabadilishwa au kupotoshwa hata herufi moja ya maandishi yake.
Tayyar Altıkulaç meongeza kuwa uchunguzi wote uliofanywa umetimia kwa kutumia nakala za digitali za kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu (SW) zilizotayarishwa na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC). Amesisitiza kuwa uchunguzi huo pia umetumia nakala za kale za Qur'ani zinazohifadhiwa katika majumba ya makumbusho ya Uzbekistan na Uturuki.
Tayyar Altıkulaç amesema matokeo ya uchunguzi huo yamehibitisha kwa mara nyingine muujiza wa kutoweza kupotoshwa kitabu cha Qur'ani na kuna umuhimu mkubwa kwa uchunguzi huo kusambazwa kwa Waislamu. 633517

captcha