IQNA

Waislamu wa Uingereza kushiriki katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds

14:24 - August 16, 2010
Habari ID: 1974315
Waislamu wa Uingereza wanapanga kushiriki kwa wingi katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yaliyopangwa kufanyika tarehe 24 Ramadhani sawa na tarehe 4 Septemba mjini London kwa shabaha ya kuonyesha uungaji mkono wao kwa wananchi madhlumu wa Palestina.
Maandamano hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Wapenzi wa Msikiti wa al-Aqsa, Taasisi ya Kiislamu barani Ulaya, Jumuiya ya Kiislamu ya Ahlul Beit (AS), Jumuiya ya Ahlul Beit (AS), Jumuiya ya Kiislamu ya Uingereza, Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Kiislamu, Umoja wa Wanachuo wa Kiislamu wa Uingereza, Jumuiya ya Umoja wa Kiislamu, Jumuiya ya Mayahudi Wanaopinga Uzayuni, Muungano wa Waislamu wa Uingereza, Umoja wa Wanachuo wa Kiislamu na Kituo cha Kurejeshwa Wakimbizi wa Palestina.
Viongozi na wasomi wa jumuiya mbalimbali za kidini na zisizo za kidini wamealikwa kuzungumza katika maandamano hayo. 633724
captcha