IQNA

Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu Duniani yalaani mzingiro wa Ghaza

18:54 - August 16, 2010
Habari ID: 1974873
Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa wa Kiislamu imelaani hatua ya Utawala wa Kizayuni ya kuendeleza mzingiro dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza kuongeza kuwa itatuma ujumbe wake kuvunja mzingiro huo.
Sheikh Ihsan Hendricks Mkuu wa Baraza Kuu la Kisheria la Waislamu Afrika Kusini ambaye pia ni mwanachama wa Baraza la Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa wa Kiislamu amesema jumuiya hiyo itatuma msafara huko Ghaza ambao utajumuisha shakhsia wa ngazi za juu wa Ulimwengu wa Kiislamu na wanafikra wa Kiarabu baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Hendriks ameashiria hali ya kusikitisha ya maisha ya watu wa Ghaza na kusema ni miaka minne sasa tokea wanajeshi wa utawala wa Kizayuni waanzisha mzingiro wao huo wa kinyama. Amesema meli msafara wa meli za Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa wa Kiislamu unakusudia kuonyesha kuwa Waisalmu kote duniani wanafungamana na Wapalestina wanaodhulumiwa hasa katika Ukanda wa Ghaza.
634616


captcha