IQNA

Visa vya Qur'ani katika lugha ya Kiingereza kwenye maonyesho ya Qur'ani mjini Tehran

12:07 - August 17, 2010
Habari ID: 1975249
Kibanda cha kimataifa cha Taasisi ya al-Mustafa (SAW) katika maonyesho ya 18 ya Qur'ani ya mjini Tehran kinaonyesha vitabu vya visa vya Qur'ani kwa lugha ya Kiingereza maalumu kwa watoto wadogo.
Kwa mujibu wa shirika la habari za Qur'ani la IQNA kutoka kwenye maonyesho hayo, visa vya Qur'ani na sira ya Mtume (SAW), visa vya mitume wengine wa Mwenyezi Mungu, visa vya hija, visa muhimu zaidi vya Qur'ani na tarjumi za Qur'ani kwa lugha ya Kiingereza ni vitabu vingine vinavyoonyeshwa katika kibanda hicho.
Kibanda hicho vilevile kinaonyesha michezo ya kumpyuta ya mafundisho ya Qur'ani na kidini kwa ajili ya kujenga vikra za watoto. 634986
captcha