Mkurugenzi wa Kitengo cha Kimataifa cha Maonyesho ya18 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Tehran Mehrdad Rakhshandeh ameiambia IQNA kwamba ufunguzi wa kitengo hicho utahudhuriwa na Mkuu wa Jumuiya ya Utamaduni na Mawasiliano ua Kiislamu ya Iran Mahdi Mustafavi na wasanii na wasomi kutoka nchi za kigeni.
Amesema kuwa wasanii hao ni kutoka nchi 15 ikiwemo Pakistan, India, Russia, Uturuki, Lebanon, Syria, Bangladesh na Thailand. Wengine ni kutoka Azerbaijan, Kyrgyzstan, Bosnia, Kuwait na Tunisia. Wasanii hao watawasilisha kazi zao za kisanii kuhusu Qur’ani katika medani ya kaligrafia na kupamba maandishi ya Qur’ani kwa maji ya dhahabu.
Mehrdad Rakhshandeh amekumbusha tena kwamba moja ya sehemu za Maonyesho ya 18 Qur’ani Tukufu ya Tehran ni kitengo cha Utamaduni wa Mataifa ya Kiislamu ambacho kitaendelea hadi mwishoni mwa maonyesho hayo. 636189