Askari hao wamekuwa wakitekeleza operesheni hizo kwa kuita na kuwahoji, bila sababu zozote za maana, shakhsia na wanaharakati wa Kishia wanaoendesha shughuli za Qur'ani katika eneo la al-Khubar nchini humo.
Ikiwa ni katika siasa hizohizo za kuwabana Waislamu wa madhehebu ya Shia, askari hao tokea mwanzoni mwa mwezi wa Ramadhani hadi sasa wamewazuia Mashia kuswali swala za jamaa nje ya mji wa al-Khubar. Watawala wa mji huo akiwemo Gavana wa Mkoa wa al-Khubar, wamekuwa wakiwaita kila wiki shakhsia mashuhuri wa Kishia wakiwemo Sayyid Muhammad Baqir na Haj Abdallah al-Muhna na kuwataka wawazuie Mashia kuswali swala za jamaa.
Awali shakhsia hao wawili mashuhuri wa Kishia walilazimishwa na askari usalama wa eneo hilo kutia saini maandishi yanayowataka wawazuie Mashia kukutana na kuswali swala za jamaa katika nyumba zao.
Tokea mwaka 2008 hadi leo askari usalama wa al-Khubar wamekuwa wakitekeleza ubaguzi na ukandamizaji wa kimadhehebu katika mji huo kwa kadiri kwamba tayari wamefunga misikiti minne ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na kuwazuia Mashia wa miji mingine ya nchi hiyo kujenga misikiti na vituo vyao vya kidini na kiutamaduni, bila kutoa sababu yoyote ya maana.
Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Saudi Arabia wanapatikana kwa wingi katika mji huo na miji mingine kadhaa ambayo ni Ihsaa, Qatif na Najran. 636234