IQNA

Chuo Kikuu cha Kwanza cha Kiislamu Marekani

15:18 - August 21, 2010
Habari ID: 1977956
Chuo Kikuu cha Kwanza cha Kiislamu kitaanzishwa pambizoni mwa Chuo Kikuu cha Berkeley California nchini Marekani.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, chuo hicho kitaanzishwa kwa jitihada za Reza Aslan, ambaye ni mhadhiri katika vyuo vikuu kadhaa vya Marekani. Imearifiwa kuwa chuo hicho hivi karibuni kitaanza kusajili wanachuo wa masomo ya muda mfupi kama hatua ya awali. Chuo hicho kitajulikana kwa jina la “Zaytuna College” na kaulimbiu yake kuu imetangazwa kuwa “Sehemu ambayo Uislamu unakutana na Marekani”
Wakuu wa elimu nchini Marekani wanasema lengo la kuasisiwa chuo hicho ni kuuarifisha Uislamu miongoni mwa Wamarekani na kuleta amani na utulivu katika jamii.
637601






captcha