IQNA

Vikao vya kidini vya Darsa za Muhammad vyaendelea nchini Algeria

11:49 - August 23, 2010
Habari ID: 1979152
Duru ya tano ya vikao vya kimataifa vya kidini vinavyofanyika chini ya anwani ya Darsa za Muhammad vimekuwa vikifanyika nchini Algeria tokea Alkhamisi tarehe 19 na vitaendelea hadi siku ya Alkhamisi tarehe Pili Septemba.
Vikao hivyo vinafanyika katika mji wa Wahran. Kikao cha ufunguzi kilihudhuriwa na Rais Abdul Azizi Boutefliqa wa Algeria pamoja na wanazuoni na maulama wa nchi za Tunisia, Morocco, Uturuki, Jordan, Syria, Sudan, Lebanon, Misri, Ufaransa na Italia.
Wasiriki wa vikao hivyo wanachambua na kuchunguza aya za Qur'ani ambazo zinazungumzia elimu ya kisasa na vilevile muujiza wa kielimu wa kitabu hicho kitakatifu. Vikao hivyo vimegawanywa katika makundi matatu ambapo wanazuoni na wasomi wa Kiislamu watashiriki katika kila kundi na kujadiliana masuala mbalimbali na wanachuo wa masuala ya kidini na kifik'hi wa Algeria.
Vilevile maonyesho ya vitabu vya Kiislamu na bidhaa za kiutamaduni yanaendelea pambizoni mwa vikao hivyo. 639080
captcha