IQNA

Maonyesho ya vitabu vya Qur'ani na kidini yafanyika Kadhimein Iraq

14:05 - August 26, 2010
Habari ID: 1981655
Maonyesho ya vitabu vya kidini, kifik'hi, kiutamaduni na vinavyohusiana na Qur'ani Tukufu yanafanyika pembeni ya haramu tukufu ya Imam Musa Kadhim (as) huko Kadhimein nchini Iraq.
Maonyesho hayo yanafanyika kwa ushirikiano wa ofisi za wanazuoni mashuhuri wa kidini na mashirika ya uchapishaji ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa shirika la Iqna, maonyesho hayo yaliyoanza siku ya Jumanne yataendelea kwa muda wa siku 10.
Taasisi nyingine zilizochangia katika kuyafanikisha maonyesho hayo ni idara za maeneo matakatifu ya Iraq zikiwemo za haramu za Imam Hussein (as), Hadharat Abbas (as), Imam Ali (as) na Imam Kadhim (as).
Vilevile kamati za kiutamaduni za ofisi za maraaji' wa kidini wa Iraq zinaonyesha katika maonyesho hayo athari na vitabu mbalimbali vya Qur'ani, vyuo vya kidini, kifik'hi, kidini na kiutamaduni. 641594
captcha