IQNA

Mashirika ya masuala ya kheri ya Kiislamu kufanya kikao Pakistan

11:35 - August 28, 2010
Habari ID: 1982382
Mashirika ya masuala ya kheri ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC yanapanga kufanya kikao maalumu huko Islamabad nchini Pakistan hapo kesho Jumapili.
Kikao hicho ambacho kitawajumuisha shakhsia mbalimbali akiwemo Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa OIC NA Ridha Gilani, Waziri Mkuu wa Pakistan kina lengo la kuchunguza hali ya wahanga zaidi ya milioni 17 ambao wameathirika kutokana na mafuriko yanayoendelea nchini humo. Kikao hicho pia kitachunguza njia za kuwasilisha misaada ya kibinadamu ambayo imetumwa nchini Pakistan na nchi za Kiislamu, kuondoa taratibu mbovu zinazotumiwa na mashirika ya misaada ya Kiislamu katika ufikishaji misaada kwa waathirika na pia kufikisha misaada hiyo kwa wakati unaofaa kwa wanaoihitaji.
Inasemekana kuwa kikao hicho pia kitachunguza uwezekano wa kuanzishwa muungano wa ushirikiano wa jumuiya za masuala ya kheri za Kiislamu. 642401
captcha