Shirika rasmi la habari la Morocco MAP limeripoti kuwa kiwanda cha uchapishaji ya Fadala ambacho kilikuwa kimefungwa kwa muda kwa sababu ya shughuli ya ukarabati pia kimefunguliwa tena.
Taasisi ya Uenezaji wa Qur'ani ya Fadala ilianzishwa kwa shabaha ya kusimamia uchapishaji wa Qur'ani Tukufu, usambambazaji wa kitabu hicho kwa njia za digitali na kugawa nakala za Qur'ani nchini Morocco na kwa raia wa nchi hiyo wanaoishi nje ya nchi.
Taasisi hiyo ambayo ina jopo la wataalamu wa masuala ya Qur'ani, pia ina jukumu la kutoa vibali vya kuchapisha na kusambaza nakala za Qur'ani nchini Morocco.
Kiwanda cha uchapishaji cha Fadala kina uwezo wa kuchapisha nakala milioni moja za Qur'ani kwa mwaka.
Kiwanda hicho kiliasisiwa mwaka 1949 na kinahesabiwa kuwa miongoni mwa viwanda vya zamani zaidi vya uchapishaji nchini Morocco.
Miradi hiyo miwili imegharibu dola milioni 10 za Kimarekani. 642448