IQNA

Mashindano ya Qurani ya wanawake ya 'Saad al Faris" Yemen yakamilika

16:18 - August 28, 2010
Habari ID: 1982857
Mashindano ya kila mwaka ya kuihifadhi Qurani Tukufu ya 'Saad al Faris' ya Yemen ambayo ni maalumu kwa wanawake na wasichana yamemalizika tarehe 27 Agosti katika mji wa Ta'izz.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Yemen, mashindano haya ya kila mwaka yamefanyika katika Ukumbi wa Taasisi ya Kitaifa na Kiutamaduni ya Vijana wa mji wa Ta'izz katika fremu ya shughuli za kila mwaka za Mwezi wa Ramadhani za taasisi hiyo.
Katika mashindano hayo washiriki 90 kutoka maeneo mbali mbali ya Yemen wameshriki katika mashindano ya viwango vya kuhifadhi Qurani kamili, kuhifadhi Juzuu 10 na Juzuu 20 za Qurani Tukufu.
Mashindano haya yanafanyika kwa mwaka wa saba mfululizo na waandalizi wanasema lengo ni kuihudumia Qurani Tukufu na kuimarisha uwezo wa wasichana na wanawake katika kuihifadhi Qurani Tukufu.
643205



captcha