Aidha katika uga wa masomo na utafiti kuhusu Qur'ani, Iran inaongoza nchi zote za Kiislamu. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Kimataifa ya Chama cha Muungano wa Kiislamu cha Iran Hamidreza Tarki alipotembelea kibanda cha Shirika la Habari la Kimataifa la Qur'ani katika Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran. Amesema maonyesho ya mwaka huu ni bora zaidi kuliko ya mwaka uliopita na kuongeza kuwa kwa ujumla shughuli za Qur'ani zinazidi kustawi nchini Iran.
Amesema juhudi zinapaswa kufanyika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata kwa njia sahali yale wanayohitajia kuhusu utafiti wa maudhui za Qur'ani Tukufu ili utamaduni wa kutekeleza mafundisho ya Qur'ani uenee katika jamii nzima. 642659