IQNA

Watoto wajifunza kusoma Qur'ani katika Maonyesho ya Qur'ani ya Tehran

11:22 - August 29, 2010
Habari ID: 1983013
Watoto wanaohudhuria Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran wanapata mafunzo ya kusoma Qur'ani katika kitengo maalumu cha watoto katika maonyesho hayo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, katika kitengo cha watoto cha Maonyesho ya Qur'ani ya Tehran kuna sehemu maalumu ijulikanayo kama “Tilawatul Qur'an” ambapo watoto wanafika hapo na kusema aya za sura mbalimbali. Imearifiwa kuwa watoto wanasoma Qur'ani huku wataalamu wa Qur'ani walio hapo wakisikiliza kwa makini na iwapo msomaji anafanya kosa anasahihishwa papo hapo na kupewa mafunzo sahihi ya tilawa.
Aidha katika kitengo hicho cha watoto kuna sehemu nyingine ijulikanayo kama “Vipimo vya Ujuzi Kuhusu Qur'ani” ambapo watoto wanaulizwa masuali mbalimbali kuhusu Qur'ani Tukufu.
Itakumbukwa kuwa Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran yalianza tarehe 27 Shaaban na yataendelea hadi tarehe 23 mwezi mtukufu wa Ramadhani.
643043
captcha