Waziri Bu Abdullah Ghulamullah amesema katika sherehe za ufunguzi kwamba mashindano hayo yanawashirikisha washindani kutoka nchi 43 duniani.
Ameongeza kuwa lego la mashindano hayo si kushinda na kupata zawadi tu bali jambo lenye umuhimu mkubwa zaidi ni kukusanyika pamoja vijana kwa ajili ya Qur'ani Tukufu na kwamba mashindano hayo ni fursa ya kutambuana wasomaji vijana wa Qur'ani Tukufu.
Waziri wa Waqfu wa Algeria amesema washindi wa kwanza hadi wa tatu wa mashindano hayo watatunukiwa zawadi nono.
Vilevile amesisitiza kuwa kandokando ya mashindano hayo kutafanyika maonyesho ya kaligrafia ya maandishi ya Qur'ani Tukufu kwa juhudi za Kituo cha Utamaduni na Masuala ya Kiislamu cha Algeria na ushirikiano wa wasanii kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Bu Abdullah Ghulamullah ameongeza kuwa sherehe za kuhitimisha mashindano hayo na kutolewa zawadi kwa washindi zitafanyika usiku wa kuamkia tarehe 27 Ramadhani.
Wizara ya Wakfu na masuala ya Kidini ya Algeria imewaalikwa pia majaji wawili wa kimataifa wa Qur'ani kutoka Iran.
Muhammad Mahdi Haqguyan, hafidhi wa Qur'ani nzima anawakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashindano hayo. 645681