IQNA

Programu ya kwanza kuhusu Uzayuni wa Kimataifa yaonyeshwa katika amonyesho ya Qur’ani Tehran

19:46 - September 02, 2010
Habari ID: 1986142
Programu ya kwanza inayohusu Mayahudi na Uzayuni wa Kimataifa inaonyeshwa katika kitengo cha Kujitenga na Maadui wa Uislamu katika Maonyesho ya 18 ya Kimataifa yanayoendelea mjini Tehran.
Programu hiyo ya CD iliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti na Sanaa cha Haniif, inajumuisha zaidi ya makala 100 na picha.
‘Marufuku kuwa Mwanamke’ , ‘Jikedume’, ‘Ukristo wa Kizayuni’, ‘Holocaust’, ‘Vyombo vya Habari’ na ‘Mfumo Mpya wa Kimataifa’ ni baadhi ya anwani za makala za programu hiyo ya CD.
Programu hiyo inayotoa picha mpya na ya matukio ya kweli kuhusu Uzayuni, itikadi na histori ya Wazauni, imepolewa kwa wingi wa watu wanaotembelea maonyesho ya Qur’ani ya Tehran.
CD hiyo pia inajumuisha vitabu 30 ambavyo majina ya baadhi yao ni: Baitul Muqaddas, Historia ya Jerusalem, Jinai ya Kimataifa, Harufu ya Damu, Vyumba vya Gesi, Ngano Zilizoasisi Uzayuni, Ujasusi wa Israel katika Darubini, Kwa nini Tunaunga Mkono Mapambano ya Intifadha, Hila za Shetani, Dunia, Mwanasesere wa Mayahudi na Udiplomasia wa Siri wa Israel katika Nchi za Kiarabu.
CD hiyo pia ina filamu nane za matukio ya kweli zinazobeba anwani za: Imam Khomeini na Kadhia ya Plestina, Labeka ya Hussein, Rachel Coory, Ukristo Uzayuni, Hadi Wakati wa Kudhihiri kwake, Mkutano wa Kufuta Ubaguzi dhidi ya Wanawake, Kimya cha Mishale ya Saa na Kibla gani? 646519

captcha