Abdul Qadir Mubarak amesema katika kikao kilichojadili shughuli za Qur’ani katika uga wa kimataifa Qur’ani kanda ya Afrika kwamba kabla ya Uislamu kuingia Madina, Mtume Mtukufu alichagua bara la Afrika na kuwatuma huko Waislamu wa awali.
Ameongeza kuwa wakati Uislamu ulikuwa bado haujafika Madina, masahaba wa Mtume Muhammad (saw) walihamia Uhabeshi Afrika kutokana na mateso waliyokuwa wakipata mjini Makka na sura ya Maryam ilikuwa ya kwanza kutarjumiwa na wahajiri hao kwa lugha ya Kiafrika.
Bwana Mubarak ameashiria pia mbinu zinazotumiwa barani Afrika kufundisha Qur’ani Tukufu na akasema, katika nchi za Afrika hususan nchi nyingi za chini ya jangwa la Sahara watoto wadogo hupelekwa madrasa za Qur’ani wakiwa bado wachanga.
Amezungumzia pia mapenzi ya Waafrika kwa Ahlubaiti wa Mtume Muhammad (saw) na nafasi ya Imam Mahdi (as) anayetambuliwa kuwa mwokozi kwa Waislamu wa Afrika hususan wafuasi wa madhehebu ya Suni na akasema licha ya kuwepo makundi ya kisalafi yanayohubiri itikadi za Kiwahabi barani Afrika, watu wa bara hilo wanawapenda vilivyo Ahlulbait na watu wa nyumba ya Mtume (as). 646596