Mashirika mawili hayo ya fedha tayari yamepeleka ombi rasmi kwa viongozi husika wa China yakiwataka washirikiane nayo katika kuanzisha benki hiyo nchini humo.
Akizungumza na waandishi habari kuhusiana na suala hilo David KP Li, mkuu wa ofisi ya uchambuzi wa kiuchumi mjini Kuala Lumpur Malaysia amesema kuwa tayari ombi hilo linachunguzwa na viongozi wa China na kuelezea matumaini yake kwamba hivi karibuni watapata jibu la kuridhisha kuhusu ombi hilo.
Taasisi ya Uwekezaji ya Malaysia Affin ina matawi katika nchi nyingi za dunia na imekuwa ikianzisha benki za Kiislamu katika nchi tofauti tokea mwaka 2006. 647052