IQNA

Mbunge mwenye chuki dhidi ya Uislamu afukuzwa kwenye chama chake Ujerumani

12:57 - September 05, 2010
Habari ID: 1987765
Thilo Sarrazin, mbunge wa Ujerumani amefukuzwa kwenye chama chake cha Social- Democrat SPD kutokana na misimamo yake mikali iliyo dhidi ya Uislamu na ya kibaguzi.
Kwa mujibu wa gazeti la Zaman la Uturuki, hivi karibuni Sarrazin aliwashambulia vikali wahajiri wa Kiislamu na Waarabu katika kitabu chake alichokipa jina la 'Ujerumani Yajitokomeza Yenyewe' akiwatuhumu kuwa ni hatari kubwa kwa usalama wa nchi hiyo.
Vilevile kwa amri ya Rais Christian Wulff wa Ujerumani mwanasiasa huyo mbaguzi alifukuzwa kutoka kwenye Jopo la Idara ya Benki Kuu ya Ujerumani kutokana na matamshi yake hayo ya kibaguzi.
Sarrazin amefukuzwa katika chama cha SPD kutokana na wingi wa kura za wanachama waliokerwa na misimamo yake ya kibaguzi. 647921
captcha