IQNA

Maonyesho ya Qur'ani Tukufu yawavutia wengi nchini Kazakhstan

18:17 - September 06, 2010
Habari ID: 1989017
Maonyesho makubwa ya Qur'ani Tukufu na nakala za maandishi ya mkono ya Kiislamu yaliyofunguliwa katika mji mkuu wa Kazakhstan Astana, yamewavutia watu wengi nchini humo.
Maonyesho hayo ambayo yanafanyika kwa mnasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani katika jumba la makumbusho la ikulu ya Rais wa Kazakhstan yanajumuisha nakala za maandishi ya mkono za Qur'ani zilizoandikwa zaidi ya karne nne zilizopita.
Vilevile maonyesho hayo yanajumuisha nakala za maandishi ya Kiislamu ya vipindi mbalimbali na katika nyanja tofauti za elimu na maarifa ya Kiislamu.
Mkuu wa kituo cha utamaduni cha Kazakhstan nchini Misri amesema kuwa nchi hiyo ilikuwa miongoni mwa ngome muhimu za elimu katika kipindi chote cha historia ya Kiislamu na ina hazina yenye thamani kubwa ya nakala za maandishi ya Kiislamu ya elimu na taaluma mbalimbali. 649346

captcha