Kikao hicho kitafanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Brussels. Kwa mujibu wa Islamic-Events, kikao hicho ambacho kimeandaliwa kwa mnasaba wa kuwadia Siku Kuu ya Idul Fitr kitaanza saa 12 na nusu hadi tatu na nusu usiku kwa wakati wa Ubelgiji. Watu waliosilimu hivi karibuni na wawakilishi wa jumuiya za Kiislamu na zisizo za Kiislamu wamealikwa kushiriki katika kikao hicho.
Lengo la kikao hicho limetajwa kuwa ni kuwapa fursa ya kujuana zaidi watu hao waliosilimu hivi karibuni, kuwajulisha wanzao ambao si Waislamu kuhusu mafundisho ya Uislamu na sababu za kusilimu kwao.
Vilevile jumuiya ya EuroIslam itatoa ripoti katika kikao hicho kuhusu mipango yake ya kueneza Uislamu barani Ulaya. Maonyesho ya kaligrafia ya wasanii na vitabu vya Kiislamu pia yatafanyika pambizoni mwa maonyesho hayo. 649571