Kituo hicho ambacho kimejengwa pembeni ya Msikiti Mkuu wa Ruyigi kwa msaada wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ulinganiaji wa Kiislamu AMAI, kilifunguliwa hiyo siku ya Jumatatu ambapo ufunguzi wake ulihudhuriwa na wanazuoni, wanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ulinganiaji wa Kiislamu nchini Burundi na wananchi Waislamu wa mji huo.
Kituo hicho kina madarasa sita ya kufundishia kuhifadhi na kusoma Qur'ani na walimu wake watakuwa wakitumwa na kudhaminiwa na jumuiya iliyotajwa ambayo ina makao makuu yake nchini Libya.
Msikiti Mkuu wa Ruyigi pia ulifunguliwa katikati ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Msikiti huo una uwezo wa kubeba wanaume 1000 na wanawake 600 na gharama ya ujenzi wake imedhaminiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Ulingajiaji wa Kiislamu.
Burundi ni nchi ndogo iliyoko katika eneo la Maziwa Makuu na inapakana na nchi za Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Tanzania. 650167