Sherehe za uzinduzi wa tarjumi hiyo ya Qur’ani yenye lugha mbili kwa pamoja zimehudhuriwa na mtawala wa Ajman Ammar bin Hamad al Nuaimi, viongozi wa serikali na shakhsia wa kiutamaduni na kidini wa Imarati.
Mtawala wa Ajman Ammar bin Hamad al Nuaimi amehutubia hadhara hiyo akisema kuwa kutarjumi na kutayarisha Qur’ani hiyo kumechukua kipindi cha miaka minne. Amesema kuwa uandishi wa tarjumi hiyo ya Qur’ani kwa lugha mbili za Kiingereza na Kifaransa ni hatua muhimu ya kueneza marifa ya Qur’ani Tukufu.
Mtawala wa eneo la Ajman huko Imarati amesema kutarjumi Qur’ani Tukufu kwa lugha zunazozungumzwa na Waislamu ndio wadhifa mkubwa zaidi wa zama hizi kwani jambo hilo linatimiza na kufanikisha kazi ya kulingania ujumbe wa Qur’ani na mafundisho ya Uislamu kote duniani. 651596