IQNA

Sheikh al Azhar alaani kuchomwa moto Qur'ani Tukufu

14:04 - September 13, 2010
Habari ID: 1992660
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al Azhar Sheikh Ahmad Tayyib amelaani hatua ya kuchomwa moto Qur'ani Tukufu huko Marekani na kusema kitendo hicho cha kishenzi hakiwezi kupunguza adhama na karama ya Mwenyezi Mungu SWT.
Sheikhul Azhar amesema Qur'ani Tukufu ni kitabu ambacho Mwenyezi Mungu mwenyewe atakilinda kama alivyosema: "Hakika Sisi ndio tulioteremsha ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutakaoulinda"
Sheikh Ahmad al Tayyb amesema Waislamu wataendelea kuheshmu dini nyinginezo lakini ameonya kuwa Waislamu kamwe hawatavumilia kuona matukufu yao yakivunjiwa heshima.
653376
captcha