IQNA

Wito wa kuchomwa Qur'ani ni kitendo cha kigaidi

14:22 - September 13, 2010
Habari ID: 1992674
Baraza la Wakristo la Iraq limetoa taarifa likilaani wito wa kuchomwa kitabu kitakatifu cha Qur'ani nchini Marekani na kusema hicho ni kitendo cha kigaidi.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Russia, baraza hilo la Wakristo wa Iraq limelaani vikali wito wa Kasisi Terry Jones wa kanisa la Dove World Outreach Center katika Jimbo la Florida wa kutaka kuchomwa Qur'ani Tukufu, wito ambao baadaye alilazimika kuufutilia mbali kutokana na mashinikizo ya Waislamu duniani.
Tarifa hiyo imesema kuwa Uislamu ni dini inayoshajiisha upndo, urafiki na udugu miongoni mwa mataifa yote duniani na kwamba wito wa kuchomwa moto kitabu hicho kitakatifu ni jinai ambayo baadhi ya watu wanaitekeleza kwa jina la demokrasia na uhuru wa kujieleza, jambo ambalo bila shaka linakwenda kinyume na mantiki ya mazungumzo baina ya dini, tamaduni na staarabu mbalimbali.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa licha ya Terry Jones kutupilia mbali uamuzi wake wa kutaka kuchoma Qur'ani, lakini baadhi ya makasisi wenye misimamo ya kupindukia mipaka na chuki dhidi ya Uislamu walichoma moto na kuchana kitabu hicho kitakatifu siku ya Jumamosi Septemba 11. Jambo hilo limekabiliwa na radiamali kali ya mamarja' wa Kishia, wanazuoni wa Kiislamu na matabaka ya Waislamu wa kawaida katika pembe mbalimbali za dunia. 652955
captcha