IQNA

Ayatullah Rafsanjani alaani kuchomwa moto Qur'ani

14:36 - September 13, 2010
Habari ID: 1992708
Mwanazuoni wa ngazi za juu wa Iran, Ayatullah Hashemi Rafsanjani ametoa taarifa akilaani vikali walioivunjia heshima Qur'ani Tukufu.
Katika taarifa hiyo amesema: "Kitendo cha kuzusha hitilafu cha kuvunjia heshima neno la Mwenyezi Mungu katika ardhi ya wanaodai kuwa ni vinara wa uhuru wa maoni ni kibaya na kiovu kiasi kwamba kinalaaniwa vikali kwa mtazamo wa kila mwanaadamu huru na dini zote.
Katika taarifa yake, Ayatullah Rafsanjani ambaye ni Mkuu wa Baraza la Wataalamu ameongeza kuwa wanaochoma moto Qur'ani wanawahudumia Wazayuni. Amesema Wamagharibi wanapanga njama dhidi ya Qur'ani Tukufu ili waweze kuzitawala nchi za Kiislamu.
Ayatullah Rafsanjani ambaye pia ni ni Mkuu wa Halmashauri ya Kuanisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu amesema Waislamu wanapaswa kuhakikisha kuwa Wamagharibi wanaangamia na njama zao hizo.
Ayatullah Rafsanjani ametoa wito kwa Umma wa Kiislamu kuwa katika hali ya tahadhari na kuchukua hatua za kuvunja njama za maadui na wawe na yakini kuwa ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kuilinda Qur'ani ni ya kweli.
653675
captcha