Kufuatia kuchomwa moto Qur'ani Tukufu katika jimbo la Florida siku ya Septemba 11, mhadhiri mmoja wa chuo kikuu cha Saudi Arabia ametaka kuanzishwa kwa chuo kikuu cha masuala ya Qur'ani katika jimbo hilo nchini Marekani.
Pendekezo hilo limetolewa na Abdul Raheem as-Salmi mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Jeddah ambaye amesisitiza kwamba kujengwa kwa chuo kikuu hicho kunaweza kuwa jibu la kuridhisha kielimu na kimantiki kwa hatua ya kasisi Terry Jones mwenye misimamo ya chuki dhidi ya mafundisho ya Uislamu katika jimbo la Florida ambaye ametaka kuchomwa moto Qur'ani. Amesema wito wa kasisi huyo wa kutaka kuchomwa Qur'ani ndio umewapelekea watu wengine walio na misimamo ya chuki dhidi ya Uislamu kuchukua hatua ya kuchoma moto kitabu hicho kitakatifu katika siku ya makumbusho ya matukio ya kigaidi ya Septremba 11 nchini Marekani. Amesema hilo litakuwa ni jibu tosha na la kimantiki kwa hatua za dharau na nyoyo zilizojaa chuki dhidi ya Qur'ani na Uislamu nchini Marekani.
As-Salmi amesema kuwa Kasisi Jones alitoa wito wa kuyakosea heshima matukufu ya Kiislamu kwa ajili ya kujipatia pesa na umashuhuri duniani na kuwataka Waislamu wakabiliane na dharau hiyo kwa njia ya mantiki na busara. 654311