Abdoulaye Wade ametoa taarifa akizitaka nchi, jumuiya, mashirika na umma mzima wa Kiislamu kukusanya misaada ya kibinadamu na kuwapelekea Wapakistan wanaokabiliwa na janga kubwa la mafuriko. Ameomboleza na familia za wahanga wa mafuriko hayo pamoja na viongozi wa serikali ya Pakistan na kuongeza kuwa anataraji nchi za Kiislamu zitachukua hatua za dharura za kutuma misaada ya kibinadamu nchini Pakistan na hivyo kuwasaidia viongozi wa nchi hiyo katika juhudi zao za kukarabati uharibifu uliosababishwa na mafuriko na vilevile kuongeza uwezo wao wa kukabiliana na magonjwa yanayotokana na mafuriko hayo.
Kwa mujibu wa takwimu za Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF, Pakistan haijawahi kushuhudia mafuriko makubwa kama hayo katika kipindi cha miaka 70 iliyopita, mafuriko ambayo hadi sasa yamewaathiri watu milioni 14 ambapo milioni sita kati yao ni watoto wadogo. 656590